
Na Waandishi Wetu/
RISASI MCHANGANYIKO
HALI inazidi kuwa mbaya kwa mastaa wawili wa muziki wa Bongo Fleva
wanaogombea unyota kimuziki, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Ali
Saleh Kiba, safari hii yameibuka mapya kwa kila msanii kuogopa kumshika
mkono mwenzake kutokana na imani za kishirikina.

Mashabiki wa Mbongofleva Ali kiba waliionyesha kumkubali zaidi kuliko, 'Daimond Platnumz' katika viwanja vya Leaders Club.
TUJIUNGE LEADERS Matukio hayo ya kusisimua
yaliwatia hofu kubwa mashabiki na wadau wa muziki Bongo muda mfupi kabla
ya nyota hao kukaribishwa stejini kwenye Viwanja vya Leaders Club,
Kinondoni jijini Dar, mwishoni mwa wiki iliyopita.
HIRIZI ZAKUTWA UWANJANI Kwa mujibu wa wanahabari
wetu, katika Viwanja vya Leaders, Kinondoni, kulikutwa hirizi
zilizozagaa, zilizodaiwa kudondoshwa na vijana waliokamatwa wakiwa
wamevalia sare zenye majina ya mastaa hao wawili.
Moja ya Hirizi iliyotupwa katika viwanja hivyo.
Katika hali ya kushangaza, mmoja wa mashabiki waliohudhuria onyesho
hilo ambaye aliziona hirizi hizo, aliwashangaza mashabiki wenzake
alipodai kuwa anaiona mojawapo ikitweta mithili ya inayopumua!
“Oneni wadau, hii hirizi si inapumua, iangalieni vizuri,” alisikika
shabiki huyo na kuwaacha watu wakiwa wamepigwa na butwaa kuona vitendo
hivyo vya kishirikina katika eneo la burudani.
Wakati matukio hayo ya kukutwa kwa hirizi
hizo yakiendelea, Diamond, baada ya kupanda jukwaani kabla ya kuanza
kuimba, akajikuta akiteleza na kuanguka jukwaani na kusimama mwenyewe
huku vijana wanaodaiwa kuwa ni wa Timu Kiba wakipiga kelele kwa nguvu
kuashiria kuwa walipendezewa na kitendo hicho kutokea.
Mashabiki waliotinga katika shoo hiyo wakishuhudia hirizi zilizo zagaa katika viwanja hivyo vya Leaders.
Pamoja na Diamond kula mwereka hadi chini, hali ilizidi kuwa mbaya
kwake baada ya muziki kuanza kusikika vibaya huku ukiwa unakatakata,
kitendo kilichoamsha hisia kuwa kulikuwa na ushirikina unaoendelea ili
kumshusha kisanii kwa kuonekana amefanya vibaya katika shoo hiyo.
CHUPA ZARUSHWA
Baada
ya kuona hali inazidi kuwa mbaya huku chupa za maji zikirushwa jukwaani
hapo na baadhi zikimpiga na nyingine akizikwepa wakati akiendelea kupiga
shoo, Diamond aliamua kutumia akili ili kuzima kelele hizo kwa kuanza
kumwaga noti.

Kikosi cha ulinzi kikiwajibika kudhibiti vijana walioonyesha tabia korofi.
Ishu hiyo iliwafanya mashabiki na Timu Kiba kuachana na zoezi hilo na
kuanza kusukumana kugombea noti hizo za elfu mbilimbili ambapo alimwaga
kwa awamu tatu.
SADAKA?
Wakati akizidi
kuwatupia noti mashabiki, Diamond alisikika akisema kuwa pesa hizo ni
maalum kwa mashabiki kwani ni sadaka kwao kutokana na sapoti kubwa
wanayompa ingawa hataweza kumpa kila mmoja.
Makamanda wa Polisi na kikosi cha Ulinzi wakihakikisha usalama unakuwepo kwa mastaa waliopangwa kutoa shoo.
DIAMOND KAMA MICHAEL JACKSON Hata hivyo, baadhi ya mashabiki waliokuwa wakisukumana na kuokota noti hizo walisikika wakisema:
“Huu mchezo alikuwa akiufanya Michael Jackson (Mwanamuziki marehemu wa
Marekani) tena alikuwa akitumia ushirikina na Freemasons.
“Michael
alikuwa anadaiwa kumwaga fedha hizo zilizokuwa na nguvu ili kuwafanya
wale waliokuwa wakimzomea kukaa kimya,” alisikika shabiki mmoja akisema.
MSHANGAO
Katika hali
ya kushangaza zaidi, Diamond alivua tisheti na vesti ya ndani na
kujifuta jasho kisha kuwarushia mashabiki huku akijua wazi kuwa amefutia
jasho lililokuwa likimiminika mwilini mwake kama maji.
Mbongofleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’
KIBA HAKUTAKIWA KUZUNGUMZA? Wakati matukio ya
kushangaza aliyokuwa akiyafanya Diamond na yale ya kurushiwa chupa za
maji machafu na yenye mikojo yakiendelea, ilidaiwa kuwa Kiba alipoingia
kwenye chumba cha wasanii hakutaka kuzungumza na mtu yeyote huku
ikidaiwa kuwa hiyo ni ishara kubwa kuwa hakutakiwa kuzungumza na mtu
kwani angeweza kupoteza nguvu za kufanya shoo.
POLISI MZIGONI Wakati mashabiki wakizidi kuwa na
wasiwasi juu ya wasanii hao, jeshi la polisi lililokuwa na zana zote za
kukamatia wahalifu, walianza doria ya kukamata vijana ambao wanadaiwa
kuwa ni Timu Kiba waliokuwa wakibishana na kutupa chupa zenye mikojo na
maji huku wakipokea kipigo kama cha mbwa mwizi.
Mbongofleva, Ali Saleh Kiba.
KIBA ARUKA UKUTA Awali kabla ya shoo hizo kuanza
matukio ya kishirikina yalijidhihirisha zaidi baada ya Ali Kiba kuingia
uwanjani hapo kwa njia ya kuruka ukuta na hata alipozama kwenye chumba
maalum walichokuwa wametengewa wasanii hakuweza kushikana mikono na
wenzake.Wasanii ambao Ali Kiba aliwachunia ni AY, MwanaFA, Shaa,
Shilole, Vanessa Mdee na Jux, ambao wote aliwakuta ndani ya chumba
hicho.
Imeandaliwa na Gladness Mallya, Musa Mateja, Chande Abdallah, Mayasa Mariwata, Shani Ramadhani, Denis Mtima na Laurent Samatta